Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akitoa maelekezo kwa
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Tabora Mhandisi Damian Ndibalinze
(mwenye koti la kijivu), mara bada ya kukagua moja boksi kalvati katika ujenzi
wa barabara ya Nyahua-Chanya yenye urefu wa KM 85.4 kwa kiwango cha lami,
mkoani humo.
Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe, akikagua kokoto
zitakazotumika katika ujenzi wa barabara ya Nyahua-Chaya yenye urefu wa KM 85.4
kwa kiwango cha lami, Mkoani Tabora.
Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akisisitiza jambo kwa
Mkandarasi kutoka kampuni ya China Henan International Cooperation (CHICO),
Mhandisi Li, mara baada ya kukagua kokoto zitakazotumika katika ujenzi wa
barabara ya Nyahua-Chanya yenye urefu wa KM 85.4 kwa kiwango cha lami, mkoani
Tabora.
Kaimu
Mhandisi Mkazi, Mhandisi Regnard Kaganga, akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, kuhusu hatua zilizofikiwa
katika mradi wa ujenzi wa barabara ya
Nyahua-Chanya yenye urefu wa KM 85.4 kwa kiwango cha lami wakati Waziri huyo
alipokuwa akikagua mradi huo, mkoani Tabora.
Muonekano
wa kazi zikiendelea za ujenzi wa tabaka la kifusi kiwango cha G7 katika
barabara ya Nyahua-Chanya yenye urefu wa KM 85.4 kwa kiwango cha lami, mkoani
Tabora. Ujenzi wa sehemu ya barabara hiyo itaunganisha mji wa Manyoni na wa Tabora.
Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe, akijadiliana jambo na
baadhi ya wafanyakazi wakati alipokuwa akikagua ujenzi wa barabara ya
Nyahua-Chaya yenye urefu wa KM 85.4 kwa kiwango cha lami, Mkoani Tabora.
Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akikagua moja ya
boksi kalvati kati ya 32 yanayojengwa katika barabara ya Nyahua-Chaya yenye
urefu wa KM 85.4 kwa kiwango cha lami,
mkoani Tabora.
PICHA
NA WUUM)
NA
WUUM, TABORA
WAZIRI
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, amemtaka
mkandarasi wa kampuni ya China Henan International Cooperation (CHICO), anayejenga
barabara ya Nyahua –Chaya yenye urefu wa KM 85.4 kukamilisha barabara hiyo
ifikapo mwezi Desemba 2020 badala ya Machi 2021.
Amezungumza hayo mkoani Tabora, wakati akikagua hatua za maendeleo ya
mradi huo unaotekelezwa kwa gharama ya shilingi bilioni 117.9 na kuridhishwa na
ubora wa kazi zilizoanza kutekelezwa.
Amemtaka mkandarasi huyo kuongeza kasi ya
ujenzi ambao umefikia asilimia 12 ikiwa
ni nyuma ya mpango kazi kwa asilimia 4.
Waziri Mhandisi Kamwelwe amesema kuwa
ujenzi wa barabara hiyo unagharamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania pamoja na Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait (KFAED) na kukamilika
kwake kutafungua mkoa wa Tabora na mikoa ya Katavi na Kigoma katika kukuza
uchumi wa wananchi.
Waziri Mhandisi Kamwelwe,
amefafanua kuwa barabara hiyo ni kiungo muhimu katika kukuza biashara na
usafirishaji wa abiria na mizigo ikiwemo inayokwenda nchi jirani.
Aidha, Waziri Kamwele ameonesha
kusikitishwa kwa vitendo vya baadhi ya wananchi kuhujumu miundombinu ya
barabara ikiwemo alama za barabarani hasa katika mkoa huo na kuomba kamati ya
ulinzi na usalama ya mkoa kusaidia Serikali katika kudhibiti.
"Kuna watu huku Tabora waliokamatwa
na vyuma vya alama za barabarani majumbani mwao wakitwangia mahindi, hili suala
halikubaliki na yeyote atakayepatikana sheria kali zitachukuliwa dhidi yake na
Serikali itaendelea kutoa elimu kwa wananchi zaidi ili kudhibiti suala
hili", amefafanua Waziri Kamwelwe.
Awali akitoa taarifa ya mradi
huo, Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Tabora Mhandisi Damian
Ndabalinze, amemueleza Waziri huyo kuwa ujenzi wa barabara hiyo utahusisha
ujenzi wa madaraja makubwa mawili, makalvati yenye pembe nne 32 na makalvati ya
mduara 60.
Akizungumzia changamoto za mradi,
Mhandisi Ndabalinze amemueleza Waziri kuwa sehemu ya mwanzo ya mradi yenye
urefu wa KM 1.7 ipo kwenye bonde ambalo kwa kipindi cha mvua za mwaka huu
lilifurika kwa zaidi ya siku saba na kusababisha kufunga barabara hiyo ambapo
eneo hilo sasa linajengewa makalvati ya pembe nne yasiyopungua saba na kujazwa
mawe kwa zaidi ya mita moja juu ya tabaka la mchanga.
Waziri Mhandisi Kamwelwe yupo
katika ziara yake ya siku tatu mkoani Tabora ikiwa ni lengo la kukagua
maendeleo ya miradi ya ujenzi wa barabara inayoendelea mkoani humo
No comments :
Post a Comment