Sunday, September 23, 2018

MAJAJI WASTAAFU MAHAKAMA KUU KANDA YA DAR ES SALAAM WAAGWA RASMI


EN7
Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi akitoa neno wakati wa hafla ya kuwaaga rasmi Majaji Wastaafu wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, walioketi ni sehemu ya Majaji Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam pamoja na Divisheni walioshiriki katika hafla hiyo.
EN1
Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi akitoa neno wakati wa hafla ya kuwaaga rasmi Majaji Wastaafu wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, walioketi ni sehemu ya Majaji Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam pamoja na Divisheni walioshiriki katika hafla hiyo.
EN2
Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu, Mhe. Sekieth Kihio akipokea zawadi kutoka kwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi, (katikati) ni Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Jaji Munisi.
EN3
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi akimpatia zawadi, Jaji Mstaafu Mhe. Laurence Kaduri ikiwa ni ishara ya pongezi kwa kumaliza utumishi wa Mahakama salama.
EN4
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi akimpatia zawadi, Mhe. Jaji Mstaafu Gadi Mjemmas
EN5
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi akimpatia zawadi, Mhe. Jaji Mstaafu Fredrica Mgaya
EN6
Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi, Mhe. Ibrahim Mipawa akitoa neno la shukrani
EN8
Jaji Kiongozi, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi (katikati) pamoja na baadhi ya Majaji wa Mahakama Kuu waliohudhuria katika hafla ya kuwaaga Majaji Wastaafu wakiwa katika picha ya pamoja na Majaji hao.
EN9
Jaji Kiongozi, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi (katikati) pamoja na baadhi ya Majaji wengine wa Mahakama Kuu waliohudhuria katika hafla wakiwa katika picha ya pamoja na Majaji Wastaafu, wa kwanza kushoto ni Jaji Mstaafu, Mhe. Sekieth Kihio, wa pili kushoto ni Jaji Mstaafu, Mhe. Laurence Kaduri, wa pili kulia ni Jaji Mstaafu, Mhe. Fredrica Mgaya, wa kwanza kulia ni Jaji Mstaafu, Mhe. Ibrahim Mipawa. Waliosimama wa pili kulia ni Jaji Mstaafu, Mhe. Gadi Mjemmas, wa pili kushoto ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Beatrice Mutungi, wa kwanza kushoto ni Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Jaji Munisi na wa kwanza kulia ni Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Ilvin Mugeta.
……………………………………………………………………………….
Na  Mary Gwera, Mahakama
JAJI Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi amewahakikishia Majaji Wastaafu kuwa Mahakama itaendelea kushirikiana nao katika masuala mbalimbali licha ya kuwa wamemaliza muda wao wa kazi.
Mhe. Jaji Feleshi aliyasema hayo, Septemba 22 jijini Dar es Salaam, katika hafla fupi ya
kuwaaga jumla ya Majaji Wastaafu tisa (9) kutoka Mahakama Kuu- Masjala Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi na Kazi.
“Napenda kuwapongeza kwa Utumishi wenu uliotukuka kwa Mahakama hadi kufikia siku ya leo, nipende kuwahakikishia kuwa Mahakama itaendelea kuwa pamoja nanyi kwa kila hali, iwe kwa shida au raha,” alisema Jaji Kiongozi.
Aidha; Mhe. Jaji Kiongozi aliwataka Majaji hao kutosita kushiriki katika shughuli mbalimbali za Mahakama ili kuendeleza maboresho ambayo Mahakama inakusudia kufikia kupitia Mpango Mkakati wake.
Aliongeza kwa kuwasihi Majaji hao Wastaafu kutosita kutoa ujuzi wao  kwa Majaji ambao bado wapo kwenye Utumishi wa Umma pindi wanapohitajika kutoa elimu katika Mafunzo mbalimbali yanayofanyika ndani ya Mahakama.
Kwa upande wake, Jaji Mstaafu, Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi, Mhe. Fredrica Mgaya ameushukuru Uongozi wa Mahakama kwa kuwaandalia hafla hiyo kwani wamefurahi na kujisikia kuwa wao bado ni sehemu ya Wanafamilia wa Mahakama.
Kwa ujumla Majaji hao Wastaafu kila mmoja kwa nafasi yake waliishukuru Mahakama ya Tanzania kwa kuwalea na kufanya kazi kwa ushirikiano katika kipindi chote cha utumishi wao.
Vilevile wametoa wito kwa Watumishi wa Mahakama ambao bado wapo kazini kufanya kazi kwa bidii na kupenda kazi zao.
Majaji Wastaafu walioagwa ni pamoja na Mhe. Sekieth Kihio, Mhe. Projestus Rugazia, Mhe. Augustine Shangwa, Mhe. Laurence Kaduri, Mhe. Gadi Mjemmas, Mhe. Fredrica Mgaya, Mhe. Ibrahim Mipawa, Mhe. Aghaton Nchimbi, na Mhe. Pelagia Khaday.

No comments :

Post a Comment