Askari
wakiweka kaburibi miili ya baadhi ya wananchi walifariki dunia katika
ajali ya Kivuko cha MV Nyerere kilichozama kwenye kisiwa cha Ukara
wilayani Ukerewe wakati wa mazishi yaliyoongozwa na Waziri Mkuu,
Kassim Majaliwa katika kijiji cha Bwisa kisiwani Bukara, Septemba 23,
2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka shada la maua kwenye kaburi la mmoja wa
wananchi walifariki katika ajali ya kivuko cha MV Nyerere kilichozama
katika katika kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe. Majaliwa aliwaongoza
mamia ya waombolezaji katika mazishi yaliyofanyika kwenye kijiji hicho
Septemba 23, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wafanyakazi
wa kujitolea na wakiungana na askari, wakiweka udongo wakati wa mazishi
ya watu waliofariki kwenye ajali ya kivuko cha Mv Nyerere, pembezoni
mwa ziwa Victoria huko Ukara, Wilayani Ukerewe Mkoani Mwanza leo
Septemba 23, 2018. (PICHA NA MICKY JAGGER WA K-VIS BLOG)
Wafanyakazi
wa Msalaba Mwekundu na askari wa ulinzi na usalama, wakishusha majeneza
yenye miili ya watu waliofariki kwenye ajali ya kuzama kwa kivuko cha
Mv Nyerere, wakati wa mazishi yaliyofanyika pembezoni mwa Ziwa Victoria
huko Ukara, Wilayani Ukerewe Mkoani Mwanza leo Septemba 23, 2018. 9PICHA
NA MICKY JAGGER WA K-VIS BLOG)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa heshima kwenye kaburi la mmoja wa
wananchi walifariki katika ajali ya kivuko cha MV Nyerere kilichozama
katika kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe. Majaliwa aliwaongoza mamia ya
waombolezaji katika mazishi yaliyofanyika kwenye kijiji hicho Septemba
23, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapa pole wafiwa katika mazishi ya mwananchi
waliofariki katika ajali ya Kivuko cha MV Nyerere kilichozama katika
kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe. Majaliwa aliwaongoza mamia ya
waombolezaji katika mazishi yaliyofanyika kwenye kijiji cha Bwisa
kisiwani Ukara Septemba 23, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Waziri wa
Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Ilemela, Angelina
Mabula na viongozi wengine walioshiriki katika mazishi ya baadhi ya
wananchi waliofariki dunia katika ajali ya meli ya MV Nyerere katika
kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe Septemba 23, 2018. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Ndugu wakiwa na huzuni wakati wa mazishi hayo. (PICHA NA K-VIS BLOG/MICKY JAGGER)
Askari wakiandaa majeneza yenye miili
ya watu waliofariki kwenye ajali yab kuzama kwa kivuko cha Mv Nyerere
tarayari kwa mazishi leo Septemba 23, 2018. (PICHA NA K-VIS BLOG/MICKY
JAGGER)
Ndugu wakiwa na huzuni wakati wa mazishi hayo. (PICHA NA K-VIS BLOG/MICKY JAGGER)
Ndugu wa marehemu wakiwa na mashada ya
maua wakati wa mazishi ya wapendwa wao leo Septemba 23, 2018. 9PICHA NA
K-VIS BLOG/MICKY JAGGER)
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohammed Abood
(wapili kulia) akiungana na Masheikh katika sala kwenye mazishi ya
wananchi waliofariki dunia katika ajali ya Kivuko cha MV Nyerere
kilichozama katika Kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe. Mazishi hayo
yaliongozwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika kijiji cha Bwisa
kisiwani Bukara, Septemba 23, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Askofu
wa Jimbo Katoliki la Bunda, Renatus Nkwande akiomba katika mazishi ya
wananchi waliofariki dunia katika ajali ya Kivuko cha MV Nyerere
kilichozama katika kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe. Mazishi hayo
yaliyoongozwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa yalifanyika katika kijiji
cha Bwisa kisiwani Bukara, Septemba 23, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza kwenye mazishi hayo. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akipewa maelezo na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John
Mongella kuhusu juhudi zinazofanywa na wahandishi za kukivuta kivuko
cha MV Nyerere kilichozama katika Kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe
wakati aliposhiriki katika mazishi ya wananchi waliokufa katika ajali ya
kivuko hicho kwenye kijiji cha Bwisa kisiwani Ukara Septemba 23, 2018.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mv Nyerere, akiwa amelala kifudifudi
huku akiacha Zaidi ya watu 225 wakipoteza Maisha. Juhudi za kukipindua
kivuko hicho zimeanza ikli kuona kama kuna miili Zaidi. 9PICHA NA OFISI
YA WAZIRI MKUU)
No comments :
Post a Comment