Thursday, July 5, 2018

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI PROFESA MBARAWA ATEMBELEA MRADI WA UBORESHAJI MIFUMO YA USAMBAZAJI MAJI INAYOSIMAMIWA NA DAWASA NA KUTOA MAAGIZO MAZITO

 Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa (katikati), akizungumza wakati wa majumuisho ya ziara yake aliyoifanya leo Julai 5, 2018 kutembelea mradi
wa uboreshaji wa mfumo wa usambazaji maji Dar es Salaam na Pwani (kushoto) ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA),
Dkt. Suphiani Masasi na kulia ni Mkandarasi wa mradi huo kutoka kampuni ya Jain Irrigation ya nchini India, Bw.Anil Vitankar.




 Muonekano wa sasa wa tanki kubwa la kuhifadhia maji e neo la Changanyikeni jijini Dar es Salaam ambapo tayari tenki hilo limeshafunikwa.
 Muonekano wa kituo cha kusukuma maji cha Salasala 
 Huu ni muonekano wa Tanki la kuhifadhia maji la Changanyikeni jijini Dar es Salaam.
 Profesa Mbarawa, akiongozana na Bi.Modester Mushi (kulia), ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa ufundi DAWASA, wakati Mhe. Waziri alipotembelea eneo la ujenzi wa kituo cha kusukuma maji cha Boko ambacho ujenzi wake umefikia hatua za mwisho.
 Profesa Mbarawa akitoa maagizo hayo.
 Bw. Anil Vitankar, wa kampuni iliyopewa kandarasi ya ujezni wa mradi huo ya Jain Irrigation, akisikiliza maagizo ya Mhe. Waziri.
Baadhi ya vifaa vya kukamilisha mradi huo vikiwa kwenye karakana huko Boko nje kidogo ya jiji
NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
WAZIRI
wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, leo Julai 5, 2018
ametembelea mradi wa uboreshaji wa mfumo wa usambazaji maji Dar es Salaam na
Pwani ambao umefikia asilimia 87.5 na kumuhimiza mkandarasi kumalizia asilimia
iliyobaki kwa wakati vinginevyo atachukua hatua kali
Profesa
Mbarawa alisema, mradi huo ambao unatekelezwa na Serikali kupitia Mamlaka ya
Mai Safi na Maji Taka (DAWASA), unathamani ya shilingi bilioni 72.43 na ni
mradi muhimu sana katika utoaji huduma kwa wananchi.
“Mkandarasi
yuko kwenye site lakini kasi yake hairidhishi, hivyo sisi kama serikali
tunajaribu kutatua kero hii ya maji kwa wananchi, lakini mkandarasi kidogo
analeta shida, kama mjuavyo mradi ulianza mwaka 2016 mwezi Machi na ulitarajiwa
kukamilika Novemba 2017 utaona tuko nyuma karibu miezi 18 tuko nyuma.” Alisema
na kutoa maelekezo
“Kwanza
tunataka uwepo kwenye site saa 24, na sio tunakuona tu lakini tuone unafanya
kazi, pili ukishinbdwa kumaliza mradi huu kama tulivyokubaliana mwezi Septemba
uelewe kwamba hii ndio itakuwa mara yako ya mwanzo na ya mwisho kupata kazi tena
hapa Tanzania, na tatu tutakutoa kwenye usajili wa chama cha makandarasi yaani
bodi ya makandarasi nah ii maana yake hutaweza kufanya kazi tena hapa Tanzania
na mwisho tutachukua Pasipoti yako ya kusafiria ili kuhakikisha kwamba unafanya
kazi na unamaliza.” Alisema.
Ziara
hiyo ya Profesa Mbarawa imemuwezsha kujionea maendeleo ya utekelezaji wa mradi
huo ulioanza Machi 2016 na unaohusisha ujenzi wa matenki matano (5) ya
kuhifadhi na kusambaza maji yenye ukubwa wa kuhifadhi lita milioni 5.0 hadi
6.0.
Pia
alitembelea ujenzi wa vituo vine (4) vya kusukuma maji vilivyo na matenki yenye
uwezo wa kuhifadhi lita milioni 3.0 kila moja, ununuzi na ufungaji wa pampu
kubwa 16 za kusukuma maji ununuzi wa transfoma na ufungaji wa njia za umeme wa
msongo mkubwa, ununuzi na ulazaji wa mabomba makubwa ya ugawaji maji na ulazaji
wa mabomba ya usambazaji maji mitaani yatakayokuwa na urefu wa jumla ya
kilomita zipatazo 477.
Kwa
mujibu wa Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Dkt. Suphiani Masasi, mradi huo utanufaisha maeneo
ya Salasala, Bunju, Wazo, Makongo, Changanyikeni, Bagamoyo, Mpiji, Zinga,
Kiromo, Kitopeni, Ukuni, Kerege, Buma, Mataya na ukanda maalum wa WPZA ambayo
ni maeneo yanayohudumiwa na mtambo wa Ruvu Chini.
Aidha
mradi pia utanufaisha maeneo yaliyopo kati ya Mbezi Louis na Kiluvya ambayo ni
Kiluvya yenyewe, Kibamba, Mbezi, Msakuzi, Makabe, Malamba- mawili na Msigani na
maeneo haya yanapata maji kutoka Mtambo wa Ruvu Juu ambao ulizinduliwa na
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanania Juni 2, 2017.
Mtendaji Mkuu huyo wa DAWASA alimueleza Mhe. Waziri kuwa lengo la mradi ni pamoja na
kuhakikisha kuwa wananchi wa kawaida wenye viwanda na biashara katika eneo lote
la mradi wanapata huduma bora za maji hasa baada ya maji kuongezeka kufuatia
kukamilika kwa kazi za upanuzi wa mitambo ya maji Ruvu Juu na Ruvu Chini.

No comments :

Post a Comment