Monday, June 11, 2018

Mobisol yazindua TV kubwa zaidi inayotumia umeme wa jua katika soko la Tanzania


MOB ARUSHA 1
Mshauri wa Masoko wa Kampuni ya nishati ya nguvu ya jua Mobisol,Livinus Manyanga, akikata utepe kuzindua luninga  kubwa inayotumia umeme wa juakwenye moja ya maduka yao jijini Arusha,wengine pichani ni Maofisa waandamizi wa kampuni hiyo.
MOBISOL 6
Meneja Masoko wa Mobisol,Seth Matemu akionyesha bidhaa bora za kampuni hiyo
MOBISOL ARUSHA 5 MOBISOL ARUSHA 8 MOBISOL ARUSHA 10
Mshauri wa Masoko wa Kampuni ya nishati ya nguvu ya jua Mobisol,Livinus Manyanga,akiongea na waandishi wa habari
…………………………………………………………………..
  Katika kukidhi mahitaji ya wateja wake wanaoishi maeneo yasio na umeme wanaohitaji televisheni kubwa,kampuni inayoongoza kwa kutoa huduma za umeme wa jua na kuuza bidhaa bora zinazotumia nishati hiyo, Kampuni ya Mobisol  imezindua televisheni bapa kubwa yenye kioo
cha kisasa ya Inchi 43 katika soko la Tanzania.
Televisheni yenye ukubwa huu na inayotumia umeme unaotokana na nishati ya jua ni kwa mara ya kwanza, imezinduliwa katika soko la Tanzania, kwa ajili ya kuwapatia burudani watumiaji wa  umeme wa jua .
Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Mobisol Tanzania,Patrick Juma,amesema kuzinduliwa kwa televisheni kubwa na ya kisasa  katika soko la Tanzania ni mwendelezo wa dhamira ya kampuni  ya kutoa huduma bora za umeme wa nishati ya jua , na kuuza bidhaa bora zinazotumia bidhaa hiyo.Aliongeza kuwa tayari televisheni hiyo kubwa kuanzia sasa inapatikana katika vituo vyote vya mauzo vya kampuni nchini kote.
Juma, alisema bidhaa hii mpya inapatikana ikiwa imeunganishwa pamoja na mtambo wa Sola Watti  200, kuhakikisha kuwa inafanya kazi kwa zaidi ya masaa 10 ,pia inakuja nakifurushi chenye taa nne,redio na tochi-vyote upatikanaji wake umewekwa katika mfumo unaowezesha wateja kumudu kuzinunua kwa kulipia kidogo kidogo.Pia mteja atakayenunua televisheni kubwa atanufaika kwa huduma mbalimbali ikiwemo  kuunganishiwa bure,atapata waranti na kuweza kuchagua huduma za televisheni ya kulipia anayoitaka.Ofa hii kubwa kwa wateja yenye kuleta burudani kwa pamoja ya matumizi ya vifaa vya kisasa vinavyotolewa na Mobisol kwa kushirikiana na kampuni ya StarTimes.
Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Mobisol Tanzania,Patrick Juma anasema “Tunajivunia kuendelea kuongoza kwa huduma na bidhaa zinazotumia umeme wa jua zenye ubora na za kisasa na kufanikisha ndoto kubwa za watumiaji wa umeme wa nishati ya jua,hususani wamiliki wa biashara na kwa matumzi ya nyumbani sehemu za mijini ambao wanahitaji bidhaa kwa kadri ya matumizi yao na mitindo yao ya maisha.Televisheni sio kifaa cha burudani tu bali pia kinawezesha kupata maarifa sambamba na kuingiza kipato kwa wanaokitumia kibiashara iwe kwenye mabaa,migahawa,mashuleni na vituo vya elimu,na kwa matumizi ya kifamilia.’’
Pia Televisheni hii ya Inchi 43 imepata kuthibitishwa kimataifa na kampuni ya Lighting Global yenye dhamana ya kuhakikisha ubora wa hali ya juu katika mitambo na vifaa vya sola vinavyotengenezwa.
Mobisol mpaka sasa imefanikiwa kuweka umeme  wenye nguvu za 10MW na kuunganisha familia zaidi ya 500,000 kwenye mtandao wake katika kanda ya nchi za Afrika Mashariki kwa gharama nafuu,ubora wa hali ya juu na unaowezesha matumizi ya kibiashara.Kwa umeme wake wa ukubwa kuanzia mitambo ya Watii 40 mpaka Watti 200,Mobisol imewezesha matumzi ya umeme kuanzia kuwasha taa,kuchaji simu,pia matumizi ya vifaa vikubwa ,bora na vya kisasa vinavyotumia umeme wa jua kama redio, Mobichaja na Televisheni.

No comments :

Post a Comment