Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Prof. Adolf Mkenda (kulia) akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la
Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini, Bw. Michael Dunford alipofika
Wizarani kwa ajili ya kuzungumzia masuala mbalimbali kuhusu utekelezaji
wa majukumu unaofanywa na Shirika hilo hapa nchini. Pamoja na mambo
mengine Mwakilishi huyo aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano
mkubwa anaopata katika kutekeleza majukumu yake. Shirika la WFP hapa
nchini linajishughulisha katika kusaidia miradi mbalimbali ya kilimo
katika kuwajengea uwezo wakulima wadogo, lishe na kusaidia upatikanaji
wa soko kwa wakulima wadogo. |
No comments :
Post a Comment