Kamishna Jenerali wa Magereza,
Dkt. Juma Malewa akiongoza kikao kazi cha Makamishna na Manaibu Kamishna
wa Magereza Ofsini kwake leo Jumatatu 11, 2018 jijini Dar es Salaam.
Jumla ya Maafisa 9 wa ngazi ya juu ya Jeshi la Magereza wamepandishwa
vyeo hivyo hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. John Pombe Magufuli kujaza nafasi mbalimbali zilizokuwa wazi ndani
ya Jeshi hilo.
Kamishna wa Fedha na Utawala wa
Magereza, Gaston Sanga(wa kwanza kulia) akiwa na Makamishna wapya wa
Jeshi hilo wakifuatilia kwa makini kikao kazi kilichoongozwa chini ya
Uenyekiti wa Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(hayupo
pichani), leo Jumatatu 11, 2018, Jijini Da es Salaam.
Manaibu Kamishna wapya wa Magereza
waliopandishwa vyeo hivyo hivi karibuni na Mhe. Rais Magufuli
wakifuatilia kikao kazi kilichoongozwa chini ya Uenyekiti wa Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini kama inavyoonekana katika picha
Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza
No comments :
Post a Comment