Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi
wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama-Lushoto (IJA), Jaji Mstaafu, Mhe. John
Mrosso akiongea jambo na Wadau walioshiriki katika kikao hicho, katikati
ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma, kushoto ni Jaji
Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali.
Wajumbe wakimsikiliza Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo, alipokuwa akielezea kuhusu Chuo hicho.
Wajumbe wa Kikao walioshiriki
ni Wawakilishi kutoka Chuo cha Dar es Salaam, Chuo cha Magereza-Kiwira,
Chuo Kikuu cha Mzumbe, Ofisi ya Utumishi na Utawala Bora,Chuo cha Kodi
n.k, Washiriki wakifuatilia kwa makini, katika kikao hicho Chuo cha
Uongozi wa Mahakama kwa kushirikiana na Mahakama ya Tanzania wamechukua
maoni yote yaliyotolewa na Wadau hao na wameahidi kuyafanyia kazi katika
kuboresha Mafunzo yanayotolewa na Chuo hicho kwa manufaa ya Watumishi
wa Mahakama na Wananchi kwa ujumla.
Baadhi ya Wajumbe wa Kikao
walioshiriki ni Wawakilishi kutoka Chuo cha Dar es Salaam, Chuo cha
Magereza-Kiwira, Chuo Kikuu cha Mzumbe, Ofisi ya Utumishi na Utawala
Bora,Chuo cha Kodi n.k, aliyeketi nyuma wa kwanza kushoto ni Jaji wa
Mahakama ya Rufani ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya
Mafunzo-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Shaaban Lila.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe.
Prof. Ibrahim Hamis Juma akifungua Kikao cha Wadau Kujadili kazi ya
ulinganisho wa chuo cha Uongozi wa Mahakama-Lushoto (IJA) na Vyuo
vingine vya Mafunzo endelevu. Kikao hicho kati ya Chuo cha Uongozi wa
Mahakama na Wadau wa Vyuo vingine vinavyotoa mafunzo endelevu kimelenga
katika kujadili uzoefu na nafasi ya ushirikiano wa karibu baina ya Chuo
hicho na Vyuo vingine vya Umma vinavyotoa mafunzo endelevu kwa Watumishi
wa umma na Wadau mbalimbali katika Sekta ya Sheria, kikao hicho
kilifanyika Aprili 16 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwl. Nyerere jijini
Dar es Salaam.
Picha ya pamoja ya ushiriki:
aliyeketi katikati ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis
Juma, wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha
Uongozi wa Mahakama-Lushoto (IJA), Jaji Mstaafu, Mhe. John Mrosso, wa
pili kushoto ni Jaji wa Mahakama ya Rufani ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Kamati ya Mafunzo-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Shaaban Lila, wa kwanza
kulia ni Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali
na wa kwanza kushoto ni Mhe. Jaji Dkt. Paul Kihwelo, Mkuu wa Chuo cha
Uongozi wa Mahakama-Lushoto (IJA).
(Picha na Mary Gwera, Mahakama)
No comments :
Post a Comment