Friday, March 23, 2018

SHIRIKA LA AGPAHI LAKABIDHI MASHINE YA KUCHUNGUZA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI KWA WANAWAKE KWA WILAYANI MUHEZA



Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dr.Sekela Mwakyusa kushoto
akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Muheza MwanashaTumbo mashine ya
kuchunguza saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake(cryotherapy
machine) kushoto anayeshuhudia ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa

Tanga,Dkt Asha Mahita


Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dr.Sekela Mwakyusa
akimpongezwa na Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mhandisi Mwanasha Tumbo mara
baada ya makabidhiano hayo kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa

Tanga,Dkt Asha Mahita

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dr.Sekela Mwakyusa katikati
akiwasikiliza kwa umakini Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Dkt Asha Mahita
na kulia ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Monica Kinala

SHIRIKA la AGPAHI linalojihusisha na masuala ya ukimwi katika kutambua
mchango wa sekta ya afya katika ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Muheza
limemkabidhi mkuu wa wilaya ya Muheza Mwanaasha Tumbo mashine ya
kuchunguza saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake( cryotherapy
machine).
Mashine hiyo mkuu wa wilaya ya Muheza alikabidhiwa
juzi na mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kwa niaba ya mkuu wa
mkoa wa Tanga Martine Shigella katika warsha ya siku mbili ya wadau wa
sekta ya ukimwi kutoka taasisi binafsi na serikali iliyofanyika katika
ukumbi wa Regal Naivera jijini Tanga juzi.

Mkurugenzi mtendaji
wa Shirika hilo hiyo Dr.Sekela Mwakyusa alisema kuwa katika kutambua
mchango wa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na mkuu huyo wa
wilaya ya Muheza katika harakati za ujenzi wa hospitali ya wilaya ya
Muheza waliamua kumzawadia mashine hiyo ikiwa ni sehemu ya mchango wao
katika vifaa tiba.

“Sisi AGPAHI leo tunakukabidhi mashine hii
ya kuchunguza saratani ya shingo ya kizazi kama sehemu ya mchango wetu
katika harakati za ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Muheza” alisema
Mwakyusa.

Kwa upande wake mkuu huyo wa wilaya alilishukuru
shirika hilo hiyo kwa kumzawadia kifaa hicho muhimu ambapo kwa kuanza
atakikabidhi katika hospitali Teule ya Muheza( Muheza DDH) ili ianze
kazi.

Hata hivyo aliwashukuru shirika la AGPAHI kwa kunipatia
kifaa hiki muhimu kwa wakina mama,nikisema kikae mpaka hospitali
ikamilike kitaharibika hivyo nitawakabidhi hospitali Teule ya Muheza ili
waanze kukitumia” alisema.

Kwa kuanzia mkuu huyo wa wilaya
alimuomba mganga mkuu wa mkoa kupanga siku maalum ya upimaji wa saratani
ya kizazi wilayani Muheza ili wakinamama wote wa mkoa wa Tanga wapate
huduma hiyo.
(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

No comments :

Post a Comment