Waziri wa Wizara ya Katiba na
Sheria Mhe. Palamagamba Kabudi amesema Wizara yake pamoja na Taasisi
zilizo chini ya Wizara hiyo imeendelea kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya
Chama cha Mapinduzi katika sekta ya sheria, ambapo pamoja na mambo
mengine, wananchi wanauelewa mkubwa wa namna ya kutafuta na kupata haki
yao kisheria. Ameyasema hayomwishoni mwa wiki wakati alipokuwa
akiwasilisha Mpango na Makadirioya Bajeti ya Wizara hiyo na Taasisi
zake kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria.Pamoja naye
ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk. Adelardus Kilangi
……………….
Na Maura Mwingira, Dodoma
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe.
Palamagamba Kabudi ( Mb) amesema, Wizara yake pamoja na Taasisi ambazo
zipo chini yake, imeendelea kutekeleza ahadi zote za Ilani ya
Chama cha
Mapinduzi zinazoambatana na na matarajio ya wananchi kutoka kwenye
sekta ya sheria.
Waziri Kabudi ameyasema hayo
mwishoni mwa wiki, wakati alipokuwa akiwasilisha Mpango na Makadirio ya
Bajeti ya Wizara hiyo na Taasisi zake mbele ya Wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria mjini Dodoma.
“Wizara yangu imekuwa ikiwajibika
vilivyo katika kuhakikisha kuwa inatekeleza ahadi zote za Ilani
zinazoambatana na matarajio ya wananchi kutoka kwenye sekta ya sheria”
ameeleza Mhe. Waziri
Akazitaja ahadi hizo kati ya
nyingi, kuwa ni, kuendeleza vita dhidi ya adui rushwa na ubathirifu wa
mali ya umma, kukuza, kulinda haki za binadamu na utawala wa sheria
katika ngazi zote za uongozi, kuimarisha mfumo wa utoaji wa haki na
kukamilisha mchakato wa Katiba mpya.
Akiwasilisha Mpango na Bajeti ya
Wizara na Taasisi zake nane, Waziri aliiomba Kamati hiyo kupitisha
zaidi ya Sh. 183.223.058,000bn/- zikiwa ni fedha za mishahara,
matumizi mengineyo na miradi ya maendeleo kwa Wizara na Taasisi zake.
Pamoja na kuwasilisha Mpango na
Makadirio ya bajeti kwa mwaka 20018/2019, Waziri Kabudi alianisha
baadhi ya mafanikio ya Wizara hiyo na taasisi zake katika bajeti ya
2017/2018.
Ameyataja baadhi ya mafanikio hayo
kuwa ni pamoja na wananchi kupata haki zao kwa wakati kutokana na
kupungua kwa mlundikano wa mashauri katika mahakama ya Tanzania kufika
chini ya asilimia kumi.
“Mhe. Mwenyekiti mafanikio
yaliyopatikana kutokana na utekelezaji wa vipaumbele hadi kufikia tobo
ya tatu ya mwaka wa fedha 2017/2018 na kwa kuzingatia Ilani ya Chama
cha Mapinduzi, ni pamoja na kuimarisha mifumo ya ulinzi na matumizi ya
utajiri na rasilimali za nchi kutokana na kuwekewa miongozo ya
kisheria” akabainisha Waziri Kabudi.
Akayataja mafanikio mengine kuwa
ni huduma za mahakama kutolewa karibu zaidi na wananchi kwa kujengwa
kwa mahakama mpya, kuimarika na kukua kwa mifumo ya ufikiaji wa haki za
kisheria na haki za binadamu, kuendelea kuimarika kwa viwango vya
usajili kitaifa hususani kwa watoto wa umri chini ya miaka miaka mitano.
Mafanikio mengine ambayo Mhe
Waziri ameyaelezea wakati wa uwasilishaji wa Mpango na Makadirio ya
Bajeti kuwa ni pamoja na, kuogezeka kwa uelewa wa wananchi kuhusu haki
zao, namna ya kudai haki zao na uwezo wa serikali katika kuwapatia
huduma ya msaada wa kisheria.
Kama hiyo haitoshi, Mhe Waziri
Kabudi ameileza Kamati kwamba, katika utekelezaji wa mpango na bajeti
ya mwaka 2017/2018, Wizara kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, katika uendeshaji wa mashauri ya daawa ( madai) hadi kufika
mwezi february 2018,ili pata ushindi katika mashauri 82 yaliyokuwa na
thamani ya shilingi 1,064,581,955,743bn/-.
Kwa mujibu wa Waziri wa Katiba na
Sheria ushindi huo umewezesha pamoja na mambo mengine, maamuzi ya
serikali pamoja na sheria za nchi kutobadilishwa kwa msingi ya kuikuka
Katiba.
Mafanikio mengine ambayo
yametajwa na Waziri Kabudi ni pamoja na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa
Serikali kama sehemu ya utelelezaji wa Ilani ya CCM,kuendelea na utoaji
wa ushauri wa kisheria kwenye mikataba na makubaliano mbalimbali
yanayofanywa na Wizara Idara na Taasisi za Serikali .
Katika eneo hilo , hadi kufikia
mwezi February, 2018 Ofisi ya Mwanasheria Mkuu ilifanya uhakiki na
kutoa ushauri wa mikataba 691 yenye thamani ya Shilingi
1,720,026,713,823bn/- na Dola za Kimarekani 1,0884,472,366, mikataba hii
ilihusu ununuzi , ukarabati wa majengo, utoaji wa huduma za jamii na
ujenzi wa barabara.
Katika uendeshaji wa kesi za
jinai, Waziri wa Katiba na Sheria aliieleza Kamati ya kudumu ya Bunge
ya Katiba na Sheria kwamba, katika kipindi kinachoishia February 2018.
Ofisi ya Taifa ya Mashtaka iliendelea na uratibu wa shughuli za
upelelezi wa makosa ya jinai mahakamani
Mashauri ya jinai
yaliyoshughulikiwa ni pamoja na yaliyohusu wanyamapori, dawa za kulevya,
uhujumu uchumi, rushwa na mauaji. Ambapo washtakiwa waliotiwa hatiani
walipewa adhabu mbalimbali zikiwamo vifungo, faini na mali kutaifishwa
ambapo jumla ya shilingi za kitanzania 2,169 ,983,500 zilitozwa kama
faini kutoka kwa washtakiwa.
Aidha kwa upande wa mali
zilizotaifishwa ni pamoja na kilogramu 24.5 za dhahabu yenye thamani ya
Shilingi 2,012,357,164 na fedha za kigeni kutoka mataifa 15 zenye
thamani ya shilingi 908,019,979. Mali nyingine zilizotaifishwa ni pamoja
na magari matano ya kifahari aina ya Range Rover Vogue na moja aina ya
Audi yaliyokamatwa katika banari ya Dare s Salaam yakisafirishwa kama
nguo za mitumba.
Mali nyingine zilizotaifishwa
katika kipindi hicho ni pikipiki, mifugo, mafuta na basi la abiria
lililokuwa likitumika kusaifirishia meno ya tembo yanazokadiriwa kuwa
na thamani ya jumla ya shilingi 3,242,787, 915.
Kwa upande wa uandishi wa Sheria,
Wizara kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, iliandaa jumla ya
miswaada 15 ya sheria ambayo iliwasilishwa Bungeni na kupitishwa na
kuwa sheria. Hali kadharika, iliadaa sheria ndogo na matamko mbalimbali
ya serikali yapatayo 164 ambayo yalichapishwa kwenye gazeti la
serikali.
Mafanikio mengine ni pamoja na kuanzishwa kwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali.
Katika kikao cha Ijumaa mafungu
yaliyopitishwa na Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Sheria na Katiba ni yale
ya Wizara, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Wakili Mkuu
na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka .
Kikao hicho cha uwasilishaji wa
mpango na bajeti ya Wizara kilihudhuriwa pia na Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, Dk. Adelardus Kilangi, Katibu Mkuu Profesa Sifuni Mchome ,
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Paul Ngwembe, Mkurugenzi Mkuu Ofisi
ya Taifa ya Mashtaka Bw. Biswalo Mganga, pamoja na wawakilishi kutoka
Taasisi nyingine zilizo chini ya Wizara ya Katiba na Sheria.
Taasisi ambazo zipo chini ya
Wizara ya Katiba na Sheria ni Mahakama ya Tanzania, Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Ofisi ya
Wakili Mkuu wa Serikali, Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini, Tume ya
Haki za Binadamu na Utawala Bora, Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania,
Tume ya Utumishi wa Mahakama, Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa
Vitendo na Chuo cha Uongozi wa Mahakama-Lushoto.
No comments :
Post a Comment