Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt.Augustine Mahiga akizungumza na Wabunge wa EALA (hawapo pichani) |
Katika ziara hii Wabunge wanatembelea miradi inayotekelezwa katika ushoroba wa kati (central corridor) sambamba
na kubaini changamoto zinazoikabili miradi hiyo na namna inavyorahisha
utoaji huduma kwa wananchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Katika
mazungumzo yao na Waziri Mahiga, Wabunge wa EALA wameipongeza Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa utekelezaji mzuri wa miradi
inayotokana na makubaliano ya Jumuiya kama vile ujenzi wa mizani za
kisasa sambamba na kupunguza idadi ya mizani hiyo ili kurahisisha
usafirishaji wa bidhaa, hudumu na watu ndani Jumuiya.
Hadi sasa Tanzania kwa upande wa ushoroba wa kati imefanikiwa kupunguza idadi ya vituo vya mizani kutoka vituo saba hadi vitatu.
Kwa
upande wake Waziri Mahiga, amewapongeza Wabunge wa EALA kwa kuona
umuhimu wa kutembelea miradi ya Jumuiya inayotekelezwa na nchi Wanachama
ambayo inagusa maisha ya wananchi moja kwa moja. Aidha amesema katika
ziara hii Wabunge wataweza kubaini changamoto zinazowakabili wananchi,
hivyo kuwa katika nafasi nzuri ya kuweza kutatua changamoto hizo wakati
wa utekelezaji wa majukumu yao Bungeni.
Mhe. Adam Kimbisa Mbunge wa EALA (Tanzania) akizungumza wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari |
No comments :
Post a Comment