Naibu
Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye akiteremka kwenye boti katika ziara yake ya
kukagua huduma za mawasiliano na maeneo ya kujenga bandari kwenye mwambao wa
Ziwa Nyasa aliyoifanya kuanzia kata ya Manda iliyopo wilayani Ludewa mkoani
Njombe hadi Itungi wiliyani Kyela mkoani Mbeya
Meneja
wa Bandari za Ziwa Nyasa Bwana Ajuaye Heri Sese (wa pili kushoto) akifafanua
jambo kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kulia) wakati wa ziara
yake kuanzia kata ya Manda iliyopo wilayani Ludewa mkoani Njombe hadi Itungi
wiliyani Kyela mkoani Mbeya. Wa kwanza kulia ni Mbunge wa Jimbo la Ludewa Mhe.
Deo Ngalawa na wa kwanza kushoto ni Katibu wa Mhe. Nditiye Mhandisi Hamza
Faiswary.
Naibu
Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (aliyeketi) akisimikwa kuwa Chifu wa kitongoji
cha Ihiiga kilichopo kwenye kijiji cha Nkwimbili, kata ya Lupingu, Wilaya ya
Ludewa iliyopo mkoani Njombe ikiwa ishara ya pongezi kwa kiongozi wa kitaifa
kufika hapo tangu mwaka 1979 katika ziara yake ya kukagua huduma za mawasiliano
na maeneo ya kujenga bandari kwenye mwambao wa Ziwa Nyasa aliyoifanya kuanzia
kata ya Manda iliyopo wilayani Ludewa mkoani Njombe hadi Itungi wiliyani Kyela
mkoani Mbeya. Wa kwanza kushoto ni mzee Thadei Otmari Ngalawa na aliyevaa
miwani ni Diwani wa Kata ya Lupingu Mhe. Skanda Mwinuka.
Naibu
Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nsele
kilichopo kata ya Kilondo wilayani Ludewa mkoani Njombe katika ziara yake ya
kukagua huduma za mawasiliano na maeneo ya kujenga bandari kwenye mwambao wa
Ziwa Nyasa aliyoifanya kuanzia kata ya Manda iliyopo wilayani Ludewa mkoani
Njombe hadi Itungi wilayani Kyela mkoani Mbeya
No comments :
Post a Comment