Sunday, February 18, 2018

LUKAKU AIPELEKA MAN U ROBO FAINALI YA KOMBE LA FA

Romelu Lukaku amefunga mara mbili wakati Manchester United ikiifunga Huddersfield kwa magoli 2-0 na kutinga robo fainali ya kombe la FA.

Mshambuliaji huyo raia wa Ubelgiji alifunga goli la kwanza katika dakika ya tatu tu ya mchezo, akiuwahi mpira wa kupenyezewa na Juan Mata.
Lukaku alifunga goli lake la 21 katika msimu huu katika kipindi cha pili baada ya kuwatoka kasi mabeki wa Huddersfield na kuwahi pasi ya Alexis Sanchez.
     Romelu Lukaku akimpoteza mahesabu kipa Jonas Lossl na kupachika goli la kwanza
   Romelu Lukaku tena akiachia shuti na kufunga goli la pili katika mchezo huo wa Kombe la FA

No comments :

Post a Comment