Tuesday, January 23, 2018

DAWASCO WAANZA UKARABATI WA BOMBA VINGUNGUTI

Siku moja baada ya ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Suleiman Jafo kukagua miradi ya maendeleo na kuagiza Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kuhakikisha mabomba ya barabara ya Buguruni kwa Mnyamani yanaanza kutengenezwa mara moja,  Hatimaye Dawasco imechukua hatua na kuanza kutekeleza agizo hilo.
Kazi hiyo imeanza mapema Jana Jioni ikihusisha wataalamu waandamizi kutoka Dawasco kukagua na kuanza hatua za awali za ubadilishaji wa bomba kubwa lenye ukubwa wa inchi 10 na kuweka bomba jipya.
Kazi hiyo itaendelea leo ambapo  bado mafundi wa Dawasco wako kazini  wakiendelea na kazi.
 index2 index3

No comments :

Post a Comment