NA TIGANYA VINCENT- RS-TABORA
SERIKALI
imepiga marufuku Halmashauri zote nchini kuingia makubaliano na
Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali(NGO’S) bila kupitia na kiuhidhinishwa
na Ofisi ya Rais
, Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa( TAMISEMI ) kwa kuwa baadhi ya
mambo yamekuwa hayaendebi na vipaumbule vya Serikali ambayo nakusudia
kuwasaidia kuwasaidia wananchi.
Kauli hiyo imetolewa jana mjini Tabora na Naibu
Katibu Mkuu (ELIMU) Ofisi ya Rais , Serikali za Mitaa na Tawala za
Mikoa( TAMISEMI ) Tixon Nzunda wakati akizungumza na Watendaji na
watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Manispaa ya Tabora ,
Halmashauri za Wilaya ya Sikonge, Uyui , Kaliua na Urambo.
Alisema
kuwa kabla ya kuanza utekelezaji wa shughuli za NGO ni vema
Halmashauri zikapeleka maombi ya mashirika ambayo ...
yameomba kufanyakazi
katika maeneo yao ili Serikali inone kama kweli inaendana na vipaumbele
ambavyo imepanga katika kuboresha maisha ya watanzana ambao maisha yao
yako chini.
Nzunda
alisema mashirika hayo yamekuwa yakidai pesa ya kusaidia Watanzania
kutoka kwa wafadhili lakini matokeo yake fedha hizo zimekuwa zikiishi
kuwanufaisha watu wachache na wanapoaandika taarifa kwa watu waliowapa
fedha wadai kuwa wamewasaidia Watanzania katika miradi ya maendeleo ya
mabilioni ya fedha kumbe sio kweli imeshia mifukoni kwa wachache.
Alisema
kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inelenga kuhakikisha kuwa kama fedha
zinatolewa kwa ajili ya walemgwa ziende kusaidia eneo husika ili
kuhakikisha thamani ya fedha inaonekana kwa jami husika , kwa Serikali
na wafadhili na wafadhili husika.
Nzunda
alisema kuwa kumekuwepo na mashirika ambapo yamekuwa yakutumia mbinu ya
kuwasaidia wananchi kumbe fedha hizo zimekuwa zikiwanufaisha watu
wachache kwa kulipwa posho na mambo mengine ambayo hayana tija kwa
wananchi wa kawaida.
Alisema
Mashirika amabayo yana nia ya kweli ya kusaididia watanzania lazima
yakubaliane na viapumbe vya Serikali ili yaweze kufanya kufanya kazi
nchini vingine ni vema yakatafute nchini nyingine ya kufanya mambo yake
bila kufuata utaratibu wa nchi hisika.
Nzunda
alitoa wito kwa Halmashauri ya kuhakikisha kuwa kabla ya kuyaruhusu
Mashirika hayo yamepata kibali cha TAMISEMI ili kuepuka kisingizio cha
kuwageuza wananchi mtaji wa wache kujipatia fedha kwa maslahi binafisi.
Alisema
mashirika yamekuwa yakianda taarifa nzuri kwa wanawapa fedha kuwa
wamesaidia jamii husika kumbe hakuna kinachoonekana Zaidi ya wao
kunufaika
Nzunda
alisema kuwa Halmashauri itakayoingia makubaliano ya NGO bila kupitia
TAMISEMI watendaji wake itabika wawajibishwe kwa kusimamia maslahi ya
umma.
Naibu
Katibu Mkuu yupo katika ziara ya kikazi katika Mikoa ya Kigoma, Tabora
na Singida kwa lengo ya kuhimiza usimamizi bora wa sekta ya elimu ,
kilimo, mifugo , utawala bora na mengine mengi.
No comments :
Post a Comment