Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri ya
Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo akitoa
maelekezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa TARURA Bw. Victor Seif wakati
alipokuwa akikagua ujenzi wa barabara ya kutoka Namelock hadi Sanya
iliyopo Wilayani Kiteto Mkoani Manyara.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri ya
Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo
akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Sunya katika Wilaya ya Kiteto Mkoani
Manyara.
Ujenzi unaoendelea wa Barabara ya
Namelock hadi Sunya kwa kiwango cha Changarawe yenye urefu wa kilometa
88.1 zilizoko katika wilaya ya Kiteto, Mkoani Manyara.
………………………………………………………………………………
Angela Msimbira OR –Tamisemi Kiteto
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mheshimiwa Seleman Jafo amesitisha
mkataba wa Mkandarasi Maginga Business Holding Co. L.t.d aliyekuwa
akijenga barabara kutoka Namelock hadi Lopeltes kwa kushindwa
kumaliza ujenzi huo kwa wakati wilayani Kiteto , Mkoani Manyarai.
Akikagua barabara hiyo Mhe
Suleman Jafo amesema ...
hajarizishwa na kazi inayofanywa na Mkandarasi
Maginga Business Holding Co. Ltd ambaye anajenga barabara ya kutoka
Namelock hadi Lukelo kwa kuwa mkataba wake ulianza tangu tarehe
17/6/2017 na kupewa miezi Tisa kukamilisha kazi hiyo lakini mpaka leo
barabara yenye kilometa 44.1 imesafishwa kilometa kumi na saba, hivyo
dhamani ya kazi iliyotekelezwa hadi sasa ni asilimia saba
Amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa
TARURA Bw. Victor Seif kuhakikisha wanaongea ndani ya siku saba ili
kupata muafaka wa ujenzi wa barabara hiyo na asipojitokeza atolewe
kwenye lisiti ya wakandarasi ambao hawataruhusiwa kufanyakazi za TARURA
nchi nzima.
Amesema kuwa Ofisi ya Rais Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa imepewa dhamana ya kusimamia na
kutekeleza ujenzi wa miundombinu kwa kuona hivyo imeanzisha wakala
maalum wa kusimamia ujenzi wa barabra vijijini (Tarura) lengo likiwa ni
kusimamia ujenzi wa barabara katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa,
barabara za vjijini na mijini
“Hakutakuwa na masiahara yeyote
fedha zinazotengwa hizi zitasimamiwa kwa kiwango kisichorizisha,
Serikali haitasita kuwachukulia hatua wafanyakazi wazembe ambao hawataki
kuwafikia wananchi ili wapate huduma nzuri
Amesema barabara hiyo ya Namelock
hadi Sunya itajengwa kwa kiwango kinachotakikana na Serikali na
lengo la serikali ni kujenga barabara ili uchumi wa kiteto uweze kupanda
kutokana na miundombinu ya barabara iliyowekwa na Serikali
Amesema kuwa Maginga
construction alipewa siku ishirini na nane kwa ajili parfomance
appraisal lakini hakufanya hivyo hii inaonyesha kuwa si mwaminifu na
uwezo wake wa kufanya kazi hauendani na kiwango cha kazi
kilichotekelezwa, hivyo fedha ya serikali ingepotea na barabara ingekuwa
haipo katika ubora unaotakiwa
Amesema barabara hiyo inatumia
zaidi ya shilingi bilioni sita kwa ajili ya ujenzi wa barabara kutoka
Namelock hadi Sunya,ukilinganisha na barabara zote zilizotengenezwa
yenyyewe inatumia fedha nyingi hivyo mkandarasi ameonyesha dhahiri
kwamba hakuweza kutekeleza kazi alizopewa katika mkataba wake na
Serikali
Ameiagiza TARURA kuwaangaliwa
wakandarasi ambao si waaminifu kutokupewa tenda za ujenzi wa barabara
nchini kwa kuona kuwa serikali ndio kichaka cha wadanganyifu kwa kuwa
hivi sasa Serikali haitaji makanjanja katika suala zima la ujenzi wa
barabara nchini.
Amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa
Taruara kuhakikisha mkandarasi huyo hapati kazi yeyote ndani ya
jamhuri ya muungano wa Tanzania,na kuwaonya wakandarasi wengine
kutokufanyakazi kwa ubabaishaji bali wafanye kazi kwa weledi ili
kutimiza malengo ya serikali ya ujenzi wa miundombinu bora kwa jamii.
Aidha Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo amewaagiza
Wakuu wa Mikoa na wakuu wa Wilaya kote nchini kusimamia miradi ya
maendeleo nchini ili dhamani ya fedha inayotolewa na Serikali iendane na
dhamani ya miradi inayotekelezwa nchini.
Mhe. Jafo amesema kazi kuu ya
Wakuu wa Mikoa nchini ni kusimamia maagizo yanayotolewa na serikali
hasa katika suala zima la kusimamia maendeleo katika maeneo yao ili
fedha zinazotolewa ziendane na kazi zinazotekelezwa katika jamii
Naye Mkurugenzi Mtendaji Mkuu Bw.
Victor Seif amesema Serikali haitasita kuwachukulia hatua wakandarasi
ambao wanaenda kinyumbe na mikataba wanayopatiwa na Serikali hasa katika
suala zima la ujenzi wa miundombinu ya barabara.
Serikali ya Tanzania kupitia
Wizara ya Fedha iliingia makubaliano na shirika la kimataifa la
Maendeleo la Marekani USAID kufadhili miradi ya barabara katika wilaya
za Mvomero, Kilombero, Kongwa na Kiteto kwa mwaka wa fedha 2014/2018.
No comments :
Post a Comment