Saturday, November 18, 2017

Dkt. Mwakyembe aipongeza TAMWA kwa kuwa na wanachama wanaokidhi vigezo vya Sheria ya Habari.

PIX 1
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt Harrison Mwakyembe akizungumza na viongozi na wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) jana Jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya miaka 30 ya chama hicho.
PIX 1B PIX 2
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) Bibi Alack Mayombo akieleza mafanikio ya chama chao ikiwa ni pamoja na kupambana na ukatili wa kijinsia  jana Jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya miaka 30 ya chama hicho.
PIX 3
Mkurugenzi  wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) Bibi Edda Sanga akieleza majukumu ya chama chao jana Jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya miaka 30 ya chama hicho.
PIX 4
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt Harrison Mwakyembe  akikata utepe kuashiria  uzinduzi wa kitabu cha mafanikio tangu kuanzishwa kwa   Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) jana Jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya kutimiza  miaka  30 ya chama hicho.
PIX 5
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt Harrison Mwakyembe  akibonyeza kitufe  kuashiria  uzinduzi wa  luninga ya mtandaoni ya Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) jana Jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya kutimiza miaka 30 ya chama hicho. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali  Dkt. Hassan Abbas.
PIX 6
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt Harrison Mwakyembe akimkabidhi Tuzo ya Heshima Bibi Fatma Alloo kwa mchango wake katika  Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) jana Jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya kutimiza  miaka 30 ya chama hicho.
PIX 7
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt Harrison Mwakyembe (katikati)  akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na baadhi ya wanachama wa  Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) jana Jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya kutimiza  miaka 30 ya chama hicho. Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali  Dkt. Hassan Abbas.
…………………………………………………………………………………..
Na. Shamimu Nyaki –WHUSM.
Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe Dkt. Harrison Mwakyembe ametoa pongezi kwa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) kwa kuwa na wanachama ambao wanakidhi vigezo vilivyopo katika ...
Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 ambapo moja ya vigezo hivyo ni kuwa na Wanataaluma ya Habari wenye elimu ya kuanzia Stashahada.
Waziri Mwakyembe ameyasema hayo Jana Jijini Dar es Salaam katika sherehe za maadhimisho ya miaka 30 ya Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) ambapo amewataka wanachama hao kuendelea na juhudi zao za kukemea ukatili wa kijinsia, ndoa za utotoni, na mauaji ya vikongwe yaliyotoa sifa kubwa kwa  chama hicho.
“Nimefurahi sana kusikia kuwa wanachama wa chama hiki wanaanzia ngazi ya Stashahada kama ambavyo Sheria yetu ya Habari inavyosema kuwa ni lazima kwa mwanataaluma ya Habari kuwa na kiwango cha Elimu kinachoanzia hapo,lakini pia Serikali inatambua sana mchango wenu wa kuilemisha jamii masuala mbalimbali ikiwemo ukatili wa kijinsia endeleeni kufanya hivyo ili jamii yetu iwe jamii bora”.Alisema Mhe. Mwakyembe.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama hicho Bibi Alack Mayombo ameishukuru Serikali kwa mchango mkubwa inaotoa kwa Chama hicho pindi inapohitaji msaada na kuahidi kushirikiana na Serikali katika kuelimisha jamii hasa masuala ya Ukatili wa Kijinsia.
“Tunashukuru sana Serikali kwa jinsi inavyotuunga mkono katika juhudi zetu za kutatua changamoto zinazoikumba jamii yetu hasa mauaji ya Vikongwe,watu wenye ulemavu wa ngozi,ndoa za utotoni  pamoja na ukatili wa kijinsia mara zote tulizotoa taarifa kwa Serikali imekuwa ikichukua hatua zinazostahili”. Aliongeza Bibi  Alack.
Naye Mkurugenzi wa Chama hicho Bi Edda Sanga ameeleza kuwa kwa kipindi cha miaka 30 tangu kilipoundwa chama hicho kimefanikiwa kufanya tafiti mbalimbali ikiwemo kiwango cha Ukeketaji, Mimba za utotoni, madawa ya kulevya na athari zake katika jamii na kutoa taarifa ambayo imesaidia kupunguza matatizo hayo.
Chama hicho kilianzishwa tarehe 17 Novemba 1987 na wanahabari wanawake lengo ikiwa ni kupinga ukatili wa aina yoyote katika jamii na tayari kimeefanikiwa kwa kiasi kikubwa,Aidha chama hicho kimezindua luninga ya Mtandaoni itakayotoa taarifa mbalimbali za Ukatili wa kijinsia pamoja na mambo mengine ya kijamii.

No comments :

Post a Comment