Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kulia) akibadilishana
mawazo na Balozi wa Sweden Nchini, Katarina Rangnitt (kushoto) katika
kikao chake kilichofanyika katika Ofisi za Wizara ya Nishati na Madini
zilizopo jijini Dar es Salaam tarehe 22 Septemba, 2017. Kikao hicho
kilishirikisha wataalam kutoka Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na
Madini, na Mamlaka ya Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta
(PURA)
Sehemu ya wajumbe wa kikao hicho
wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (hayupo
pichani)
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka
ya Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta (PURA), Chalers
Sangweni (kulia) na mjiolojia kutoka mamlaka mamlaka hiyo, Simon
Nkenyeli (kushoto) wakifuatilia majadiliano mbalimbali katika kikao
hicho
Mtaalam wa Masuala ya Nishati
kutoka Ubalozi wa Sweden Nchini, Jorgen Eriksson (kushoto) akieleza
jambo katika kikao hicho. Kulia ni Balozi wa Sweden Nchini, Katarina
Rangnitt.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (katikati) na Balozi
wa Sweden Nchini, Katarina Rangnitt ( wa nne kutoka kushoto) wakiwa
katika picha ya pamoja na wajumbe wa kikao hicho.
No comments :
Post a Comment