Friday, August 18, 2017

WANAOISHI PORI TENGEFU LA LOLIONDO WATAKIWA KUONDOKA

image.php_Na Mahmoud Ahmad Arusha

Waziri wa maliasili na utalii Jumanne Maghembe amewataka wananchi wanaoishi pori tengefu la loliondo kuondoka katika pori hilo ili kupisha shughuli za uhifadhi. 
Aliyasema hayo katika Hafla ya kuwatunuku vyeti wamiliki wa hotel zinazokidhi viwango vya... ubora vya kuwalaza wageni. 
Amesema kuwa, Zipo hekari elfu mbili zilizotengwa na serikali kwa ajili ya wananchi ambazo zimeshaelekezwa huduma muhimu lakini wananchi hawataki kukaa kule. 
Maghembe amesema kuwa, wananchi wamekuwa wakidanganywa na taasisi zisizo za kiserikali kuendelea  kuishi katika maeneo ya pori tengefu la loliondo ambapo jambo hilo ni kinyume cha sheria ya uhifadhi wakati serikali ilishatenga hekari elfu mbili na mia tano kwa ajili yao. 
Akasisitiza kwamba huduma muhimu za kijamii zimeshazogezwa katika eneo hilo ambapo hadi sasa wananchi wamekuwa wakisita kuhamia katika maeneo hayo na kuendeleza maisha yao jambo ambalo serikali inawataka kuhakikisha wanahamia katika maeneo ambayo serikali imewatengea. 
Aidha aliongeza kuwa  ,Rais Magufuli alishasema Watu wenye mifugo mingi waiondoe kwenye hifadhi ama wapunguze mifugo ili wabaki na michache ya kujikimu. 

No comments :

Post a Comment