Monday, July 17, 2017

WAZIRI PROFESA NDALICHAKO AFANYA ZIARA

IMG_1647

Mheshimiwa Joyce Ndalichako  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi akizungumza na Mbunge wa Iringa mjini Mh. Mchungaji Peter Msigwa  katika Shule ya Viziwi, kulia ni Mbunge Viti Maalum Mhe Zainab Mwamwindi akisikiliza na katikati ni Mbunge wa viti Maalum Iringa Mh. Ritha Kabati.

Mheshimiwa Profesa Joyce Ndalichako  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi alifanya ziara ya ghafla katika shule Mkoani Iringa. Alitembelea shule zinazofundisha watoto wenye mahitaji maalum za Makala Wilaya ya Mfundi, Shule ya viziwi Mtwivila, Shule ya sekondari ya wasichana Mtwivila na shule ya sekondari ya Lugalo. Nia ya ziara ni pamoja na kukagua vifaa vya kufndishia ambvyo serikali imetoa. Pia alipta fursa ya kusalimia wanafunzi na walimu. Katika ziara hiyo aliongzana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe  Amina Masenza, Katibu Tawala wa mkoa wa Iringa Bi wamoja Ayoub, Wakuu wa wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Jamhuri David na Iringa Mheshimiwa Richard Kasesela. Pia wabunge waheshimiwa, Ritta Kabati, Zainab Mwamwindi na Mch Peter Msigwa
IMG_1466
Mheshimiwa Joyce Ndalichako  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Richard Kasesela kushoto ni Mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa.
IMG_1481
Mheshimiwa Joyce Ndalichako  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi akizungumza  pamoja na viongozi mbalimbali mkoani Iringa wakifurahia jambo na wanafunzi wa shule ya maalum ya viziwi mkoani humu
IMG_1855
Mheshimiwa Joyce Ndalichako  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi akizungumza na Mh. Ritha Kabati akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi
IMG_1867
Profesa Ndalichako nawanafunzi wa Iringa Girls 
IMG_1940
Profesa Ndalichako akiongea na wananfunzi wa Shule ya sekondari Lugalo kidato cha 5

No comments :

Post a Comment