Kamishna wa Kodi za Ndani wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya akiongea na
Wafanyabiashara wa Wilaya ya Uvinza kuhusu umuhimu wa kupata Namba ya
Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) wakati wa Uzinduzi wa zoezi la
uandikishaji wa Walipakodi wapya katika Wilaya hiyo Mkoani Kigoma.
Baadhi ya Wafanyabiashara wa
Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma wakipata maelezo juu ya namna ya kupata
Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) toka kwa Kamishna wa Kodi za
Ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya (hayupo
pichani) wakati wa Uzinduzi wa zoezi la uandikishaji wa Walipakodi
wapya Wilayani hapo.
Kamishna wa Kodi za Ndani wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya (aliyekaa)
akimsajili Mfanyabiashara wa Wilaya ya Uvinza, Bw. Samson Jacob ili
aweze kupata Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) wakati wa Uzinduzi
wa zoezi la uandikishaji wa Walipakodi wapya katika Wilaya hiyo Mkoani
Kigoma.
Kamishna wa Kodi za Ndani wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya (kulia)
akimkabidhi Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) mmoja wa
Wafanyabiashara wa Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma mara baada ya
kumfanyia usajili.
(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-TRA
…………………
Na Rachel Mkundai, Kigoma
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
imeendelea na kampeni yake ya kuwasajili walipakodi wapya katika maeneo
mbalimbali nchini na jana zoezi hilo limefanyika katika Wilaya ya
Uvinza, mkoani Kigoma.
Zoezi hilo ambalo liliongozwa na
Kamishna wa Kodi za Ndani wa TRA Bw. Elijah Mwandumbya ambaye amewataka
wakazi wa wilaya ya Uvinza kujitokeza kutumia fursa hiyo ambapo TRA
imewafuata kwenye maeneo yao.
“Tunaamini wengine hawajawahi
kabisa kupata namba ya utambulisho wa mlipakodi, tumeona ni vema tusogee
kwenu ili kama kuna mambo ambayo hamyaelewi mtuulize tuweze
kuwafafanulia, lakini ya ambao tumeijia hapa ni kuja kuwasajili na
kuwapatia namba ya utambulisho wa mlipakodi”, amesema Bw. Mwandumbya.
Aidha, ameongeza kuwa ili kutimiza
lengo na mikakati mbalimbali ya serikali katika kuwahudumia wananchi
lazima kodi ikusanywe na hivyo amewasihi wananchi wa Uvinza kujitokeza
kujisajili na kulipa kodi stahiki kwa mujibu wa sheria za kodi.
Naye Afisa biashara wa wilaya ya
Uvinza Bw. Godfrey Celestine amesema, hii ni fursa na neema kwa wakazi
wa wilaya hiyo kwa kuwa upatikanaji wa namba ya utambulisho wa mlipakodi
utasaidia wafanyabiashara kupata leseni za biashara kwa urahisi na
kurahisisha ufanyaji biashara na kulipakodi stahiki kwa serikali.
“Zoezi hili litawasaidia siyo tu
kupata namba ya utambulisho ya mkipakodi bali pia kupata cheti safi cha
kodi (tax clearance certificate) ambayo itawawezesha kupata leseni kwa
urahisi, nawasihi watumie fursa hii waweze kufanya biashara zao kwa
uhuru na kulipakodi”,
Nao wafanyabishara wameeleza
furaha yao kwa TRA kuwafuata mahali walipo na kuwasajili kuwa walipakodi
na wamesema kwa sasa wanajua umuhimu wa kulipakodi kwa kuwa wanaona
maendeleo yanayotokana na kodi hizo.
Mmoja wa wananchi hao Bw. Hamis
Lugoe amesema “Ni wajibu wa wafanyabishara kulipa kodi kwa kuwa kodi
ndiyo inaleta maendeleo na kuboresha maisha kwa wananchi wote hata wa
vijijini”, alisema.
Mfanyabishara mwingine aliyefika
kusajiliwa Bi. Milembe Almas amesema amewasihi wafanyabiashara wengine
kupenda kupata elimu ya kodi kabla ya kwenda kulipa kodi ili waelewe
kama yeye alivyoelewa umuhimu wa kulipakodi kwa maendeleo ya taifa.
Kabla ya kuwasajili, Kamishna
wa kodi za ndani, Bw. Mwandumbya alipata fursa ya kuwapa elimu ya kodi
wakazi wa eneo la senta katika wilaya ya Uvinza na wananchi walipata
fursa ya kuuliza maswali mbalimbali na kupata ufafanuzi wa kina
No comments :
Post a Comment