Saturday, February 17, 2018

RIYAD MAHREZ AISAIDIA LEICESTER KUTINGA ROBO FAINALI KOMBE LA FA

Timu ya Leicester City imeweka kando sakata la uhamisho wa Riyad Mahrez baada ya mchezaji huyo raia wa Algeria kuisaidia kutinga robo fainali ya Kombe la FA, kocha wa timu hiyo Claude Puel amesema.

Mahrez, ambaye alirejea kikosini baada ya kukosekana mazoezini kwa siku 10, baada ya pendekezo la kuhamia Manchester City kugonga mwamba, alimtengenezea nafasi ya kufunga mshambuliaji Jamie Vardy na kufanya matokeo kuwa 1-0 dhidi ya Sheffield United.
Mpira uliopigwa na  Jamie Vardy ukitinga wavuni na kuandika goli pekee katika mchezo huo
Jamie Vardy akifunga goli ambalo hata hivyo lilikataliwa na refa msadizi katika mchezo huo

No comments :

Post a Comment