Sunday, December 17, 2017

SHIRIKA LA FOUNDATION FOR TOMORROW LATOA TUZO MAALUMU KWA WALIMU WALIOSHIRIKI KATIKA KINYANG’ANYIRO CHA KUWASAKA WALIMU BORA MKOA WA ARUSHA

Kushoto aliyevalia koti jeusi ni Mgeni rasmi Mariam Kimoso
ambaye alimuakilisha mkurugenzi wa jiji la Arusha akimkabidhi mwalimu
aliyefanya vizuri hivi karibuni katika kinyang’anyiro cha kuwasaka walimu bora
lililoendeshwa na shirika lisilokuwa la kiserikali la Foundation For Tomorrow
jijini Arusha,katikati ni diwani wa kata ya Themi jijini Arusha,
Milance Kinabo, (CHADEMA),(Habari Picha na Pamela Mollel-Arusha)
Mkurugenzi wa shirika la Foundation for Tomorrow Melissa Queyquep, akizungumza katika hafla hiyo ambapo alisema kuwa lengo ni kuwawezesha walimu kupata mamlaka ambayo itawasaidia katika ufundishaji wa wanafunzi bila ubaguzi wowote katika kufufua maendelea ya elimu
Mgeni rasmi Mariam Kimoso
ambaye alimuakilisha mkurugenzi wa jiji la Arusha akizungumza katika hafla hiyo
 
Mjumbe wa bodi wa shirika la Foundation for Donacian Lyaruu
akizungumza katika hafla hiyo
Diwani wa kata ya Themi jijini Arusha,Milance Kinabo, (CHADEMA),akiteta jambo na Bi.Narja Roel
 Mwalimu Pius Edward kutoka shule ya msingi Sing’isi akipokea
zawadi kwa mgeni rasmi
 Mkurugenzi wa Upendo  Friends Isabella Mwampamba alisema kuwa
mwalimu anatakiwa kuheshimika kwa kazi kubwa ambayo wamekuwa wakifanya hivyo ni
muhimu sana kuwatia moyo
 Mwenyekiti wa wakuu wa shule jiji la Arusha Msendekwa
Reginard akizungumza katika hafla hiyo
 Mkurugenzi wa shirika la Foundation for Tomorrow Melissa Queyquep,akimkabidhi zawadi ya T-shirt diwani kata ya Themi jijini Arusha Milance Kinabo
  Mkurugenzi wa Upendo  Friends Isabella Mwampamba akiteta jambo na Mkurugenzi wa shirika la Foundation for Tomorrow Melissa Queyquep 
 Picha ya pamoja
Na Pamela Mollel,Arusha
Wadau mbalimbali wa elimu wametakiwa kuunga mkono juhudi
zinazofanywa na taasisi ya Foundation for tomorrow katika harakati za kuwapa...
uwezo walimu pamoja nakuwapa motisha hali ambayo itasaidia wanafunzi kufanya
vizuri zaidi wawapo mashuleni
Akizungumza hivi karibu katika Tuzo maalumu ya walimu
iliyoandaliwa na shirika lisilokuwa la kiserikali la Foundation For Tomorrow,
Mgeni rasmi Mariam Kimoso ambaye alimuakilisha mkurugenzi wa jiji la Arusha,alisema
kuwa walimu wanakazi kubwa sana hivyo ni vyema wakapongezwa kwa kazi nzuri
wanayofanya
Alisema kuwa elimu kubwa inayotolewa na walimu kwa wanafunzi
mashuleni itasaidia kuleta mandeleo na jamiii nzima itafaidika kupitia elimu
hiyo
Mkurugenzi wa shirika la
Foundation for Tomorrow Melissa Queyquep,
alisema kuwa
lengo ni kuwawezesha walimu kupata mamlaka ambayo itawasaidia katika
ufundishaji wa wanafunzi bila ubaguzi wowote katika kufukia maendelea ya elimu
“Mamlaka hayo ni kusimamia mitahala vyema huku walimu ambayo
watakaoweza kufanya hivyo kuwapongeza ili wawezekufundisha wanafunzi vyema
katika kufikia malengo endelevu kwa wanafunzi”alisema Melissa
Aidha alisema kuwa shirika hilo linalenga katika kuwapa
wanafunzi uwezo wa kuchochoea na kuchambua mawazo wawapo mashuleni,kuwasaidia
wanafunzi wanaohitahi kujifunza zaidi,
Kwa upande wake mkurugenzi wa Upendo  Friends Isabella Mwampamba alisema kuwa
mwalimu anatakiwa kuheshimika kwa kazi kubwa ambayo wamekuwa wakifanya hivyo ni
muhimu sana kuwatia moyo

No comments :

Post a Comment