Tuesday, December 12, 2017

MOHAMED SALAH ATWAA TUZO YA MCHEZAJI BORA AFRIKA YA BBC

Mshambuliaji Mohamed Salah amefanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka Afrika inayotolewa na Shirika la Utangazaji la BBC.

Mshambuliaji huyo wa Liverpool na timu ya taifa ya Misri amekuwa katika kiwango kizuri kwa klabu yake pamoja na kwa taifa lake.

Salah, ambaye alijiunga na Livepool kwa ada ya paundi milioni 39 akitokea Roma katika majira ya joto, amefanya makubwa akiwa chini ya kocha Jurgen Klopp katika msimu huu.
        Mohamed Salah akipongezwa na wachezaji wenzake wa Liverpool baada ya kufunga

No comments :

Post a Comment