Nahodha wa timu ya Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi iliyoundwa na wachezaji kutoka kutoka Jeshi la Polisi,
Magereza, Zimamoto na Uhamiaji Amina Juma Kizaba akipokea kombe la
ushindi wa kwanza kutoka kwa Mdadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania
Luteni Jenerali James A. Mwakibolwa jana Tukuyu Mbeya baada ya kuilaza
timu pinzani ya Kiimo Kijiji Kitulivu (KKR) kwa mabao 26-16.
Baadhi ya wachezaji wa timu ya
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi iliyoundwa na wachezaji kutoka kutoka
Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uhamiaji wakifurahia ubingwa wao
mara baada ya mechi jana Tukuyu Mkoani Mbeya.
Wachezaji wa timu ya Ndato wakifanya mazoezi kabla ya mechi yao dhidi ya timu ya Isange.
Wachezaji wa timu ya Ndato
(waliovaa jezi nyeupe) wakimenyanya na timu ya Isange (waliovaa jezi za
bluu) wakati wafainali ya Tamasha la Tulia Trust Tukuyu mkoani Mbeya.
Picha na Eleuteri Mangi,WHUSM, Tukuyu
………………………
Na Eleuteri Mangi, WHUSM, Tukuyu.
Washindi wa mchezo wa soka na
mpira wa pete wapokea kitita cha wamepokea kitika cha Sh. 7,500,000/=
katika Tamasha la Ngoma za ...
Jadi linaloratibiwa na Taasisi ya Tulia Trut
wilayani Tukuyu mkoa wa Mbeya.
Tamasha hilo limeifanya wilaya ya
Tukuyu kuendelea kung’ara katika tasnia ya michezo kwa kupambwa na
michezo mbalimbali ikiwemo soka, mpira wa pete na ngoma za jadi ambapo
tamasha hilo linatarajiwa kuhitimishwa Septemba 23 mwaka huu na
kuongozwa na kaulimbiu “Tuuenzi Utamaduni wetu”.
Uwanja wa Tulia ambao awali
ulikuwa unaitwa Tandale ulifurika mashabiki kutoka maeneo mbalimbali ya
mkoa huo na mikoa inayoshiriki tamasha hilo wameshuhudia timu za Ndato
na Isange zilipokutana kumenyana katika hatua ya fainali ambapo Ndato
ndio walioibuka kidedea kwa kuwalaza Isange kwa mabao 2-1.
Mchezo huo ulianza kwa kasi huku
kila timu ikitafuta bao la mapema ambapo dakika ya pili kipindi cha
kwanza Ndato ndio waliofanikiwa kupata bao la kuongoza lililofungwa na
mchezaji Monte Stephano.
Mashambulizi ya kushtukiza
yaliendelea kwa kila upande ili kutafuta ushindi, dakika ya 18 kipindi
cha kwanza Isange walipata bao la kusawazisha kupitia kapteni wake
Hussein Mwalugaja, bao lililozipeleka timu zote kwenye mapumziko kwa
kufungana goli 1-1.
Kipindi cha pili kilianza kwa vuta
nikuvute ambapo Ndato ndio walifanikiwa kupata bao la kuongoza ambapo
hadi kipenga cha mwisho Ndato ndio walioibuka kidedea kwa mabao 2-1.
Kwa upande wa mpira wa pete, timu
ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi iliyoundwa na wachezaji kutoka
kutoka Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uhamiaji waliwalaza timu
pinzani ya Kiimo Kijiji Kitulivu (KKR) kwa mabao 26-16.
Kwa ushindi huo, bingwa ambao ni
timu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imepata zawadi ya kombe, medali
na kujipatia kitita cha Sh. 1,500,000/= wakati mshindi wa pili ambaye
ni timu ya KKR nayo ikijipatia kombe, medali na kitita cha Sh.
1000,000/= huku mshindi wa tatu akijipatia sh. 750,000/= na mshindi wa
nne akiweka kibindoni sh.500,000/=
Akizungumzia tamasha hilo
linaloendelea hadi Sptemba 23 mwaka huu, Mwasisi wa Taasisi ya Tulia
Trust ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. Tulia Ackson amesema kuwa wamejipanga kulifanya tamasha
hilo kuwa endelevu na kuwa na wigo mpana zaidi na hatimaye kufikia nchi
nzima.
Dkt. Tulia Ackson amewashukuru
wadhamini kwa kufanikisha tamasha hilo na kuwa waomba waendelee kujitoa
kwa lengo la kuijenga Tanzania yenye utamaduni imara unaotoa ajira na
kulinda maadili ya Kitanzania.
Wadhamini hao ni pamoja na Benki
ya CRDB, Ubalozi wa China, Umoja wa Mataifa (UN), Ubalozi wa Ujerumani,
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Bodi ya Utalii Tanzania, PPF, WCF,
Vodacom, TCRA, pamoja na Kampuni ya TOL Gas Ltd.
No comments :
Post a Comment